Amosi 1

1 Maneno ya Amosi, mmoja wa wachunga wanyama wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda na Yeroboamu mwana wa Yoashi alipokuwa mfalme wa Israeli.

2 Alisema:

“Bwanaananguruma toka Sayuni,

pia ananguruma kutoka Yerusalemu;

malisho ya wachunga wanyama yanakauka,

kilele cha Karmeli kinanyauka.”

Hukumu Juu Ya Majirani Wa Israeli

3 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kwa dhambi tatu za Dameski,

hata kwa dhambi nne,

sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu aliipura Gileadi

kwa vyombo vya chuma vyenye meno.

4 Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli

ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi.

5 Nitalivunja lango la Dameski;

nitamwangamiza mfalme

# aliyeko katika Bonde la Aveni

na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni.

Watu wote wa Aramu watakwenda

uhamishoni huko Kiri,”

asemaBwana.

6 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kwa dhambi tatu za Gaza,

hata kwa dhambi nne,

sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima

na kuwauza kwa Edomu,

7 nitatuma moto juu ya kuta za Gaza

ambao utateketeza ngome zake.

8 Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi

na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni.

Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni,

hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,”

asemaBwanaMwenyezi.

9 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kwa dhambi tatu za Tiro,

hata kwa dhambi nne,

sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu,

na kutokujali mapatano ya undugu,

10 Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro

ambao utateketeza ngome zake.”

11 Hili ndiloBwanaasemalo:

“Kwa dhambi tatu za Edomu,

hata kwa dhambi nne,

sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga,

alikataa kuonyesha huruma yo yote,

kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote

na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.

12 Nitatuma moto juu ya Temani

ambao utateketeza maboma ya Bosra.”

13 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kwa dhambi tatu za Amoni,

hata kwa dhambi nne,

sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi

ili kuongeza mipaka yake.

14 Nitatuma moto kwenye kuta za Raba

ambao utateketeza ngome zake

katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano,

katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba.

15 Mfalme wake atakwenda uhamishoni,

yeye pamoja na maafisa wake,”

asemaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/AMO/1-bd20a9f8d7c7ee7f62bebeb1022c5061.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × five =