Amosi 3

Mashahidi Waitwa Dhidi Ya Israeli

1 Sikilizeni neno hiliBwanaalilosema dhidi yenu, Enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri:

2 “Ni ninyi tu niliowachagua

kati ya jamaa zote za dunia,

kwa hiyo nitawaadhibu

kwa ajili ya dhambi zenu zote.”

3 Je, watu wawili hutembea pamoja

wasipokubaliana kufanya hivyo?

4 Je, simba hunguruma katika kichaka

wakati hana mawindo?

Aweza kuvuma katika pango

wakati ambao hajakamata cho chote?

5 Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini

ambapo hajategewa chambo?

Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini

wakati ambapo hakuna cho chote cha kunasa?

6 Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,

watu hawatetemeki?

Mji upatwapo na maafa,

je, siBwanaamesababisha?

7 HakikaBwanaMwenyezi hatafanya neno lo lote

bila kuwafunulia watumishi wake manabii

siri yake.

8 Simba amenguruma:

je, ni nani ambaye hataogopa?

BwanaMwenyezi ametamka:

je, ni nani awezaye kunyamaza

ila kutoa unabii?

9 Tangazeni katika ngome za Ashdodi

na katika ngome za Misri:

“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;

angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,

na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.”

10 Bwanaasema: “Hawajui kutenda lililo jema,

wale ambao hujilundikia nyara

na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”

11 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanaMwenyezi:

“Adui ataizingira nchi;

ataangusha chini ngome zenu

na kuteka nyara maboma yenu.”

12 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba

vipande viwili tu vya mfupa wa mguu

au kipande cha sikio,

hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,

wale wakaao Samaria

kwenye kingo za vitanda vyao

na katika Dameski

kwenye viti vyao vya fahari.”

13 “Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana,BwanaMungu Mwenye Nguvu Zote.

14 “Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake,

nitaharibu madhabahu za Betheli;

pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali

na kuanguka chini.

15 Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,

pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;

nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu

na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”

asemaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/AMO/3-ada4971a53a7543228046864d9aa670e.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three × 4 =