Amosi 4

Israeli Hajarudi Kwa Mungu

1 Sikilizeni neno hili, ninyi ng’ombe wa Bashani

mlioko juu ya Mlima Samaria,

ninyi wanawake mnaowaonea maskini

na kuwagandamiza wahitaji

na kuwaambia wanaume wenu,

“Tuleteeni vinywaji!”

2 BwanaMwenyezi ameapa kwa utakatifu wake:

“Hakika wakati utakuja

mtakapochukuliwa na kulabu,

na wanaosalia kwa ndoana za samaki.

3 Nanyi mtakwenda moja kwa moja

kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta,

nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,”

asemaBwana.

4 “Nendeni Betheli mkatende dhambi;

nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi.

Leteni dhabihu zenu kila asubuhi,

zaka zenu kila mwaka wa tatu.

5 Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani,

jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari:

jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, Enyi Waisraeli,

kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,”

asemaBwanaMwenyezi.

6 “Niliwapa njaa kwenye kila mji

na ukosefu wa chakula katika kila mji,

hata hivyo bado hamjanirudia mimi,”

asemaBwana.

7 “Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu

kabla ya kufikia mavuno.

Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja,

lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine.

Shamba moja lilipata mvua,

na lingine halikupata nalo likakauka.

8 Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji,

lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asemaBwana.

9 “Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu,

niliyapiga kwa kutu na ukungu.

Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asemaBwana.

10 “Niliwapelekea tauni miongoni mwenu

kama nilivyofanya kule Misri.

Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga,

niliwachukua farasi wenu.

Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asemaBwana.

11 “Niliwaangamiza baadhi yenu kama

nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.

Mlikuwa kama kijiti kiwakacho

kilichonyakuliwa motoni,

hata hivyo hamjanirudia,”

asemaBwana.

12 “Kwa hiyo hili ndilo nitakalowafanyia, Israeli,

na kwa sababu nitawafanyia hili,

jiandaeni kukutana na Mungu wenu, Ee Israeli.”

13 Yeye ambaye hufanya milima,

anaumba upepo,

na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu,

yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza,

na kukanyaga mahali pa juu pa nchi:

BwanaMungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/AMO/4-eae60c5bcb1e245043031d20a6d46ed3.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 5 =