Amosi 5

Maombolezo Na Wito Wa Toba

1 Sikia neno hili, Ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi:

2 “Bikira Israeli ameanguka,

kamwe hatainuka tena,

ameachwa pweke katika nchi yake,

hakuna ye yote wa kumwinua.”

3 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani,

mia moja tu watarudi;

wakati mji utakapopeleka mia moja,

kumi tu ndio watarudi hai.”

4 Hili ndiloBwanaasemalo kwa nyumba ya Israeli:

“Nitafuteni mpate kuishi,

5 Msitafute Betheli,

msiende Gilgali,

msisafiri kwenda Beer-Sheba.

Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni,

# na Betheli itakuwa si kitu.”

6 MtafuteniBwanampate kuishi,

au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto;

utawateketeza,

nayo Betheli haitakuwa

na ye yote wa kuuzima.

7 Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu

na kuiangusha haki chini

8 (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni,

ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko

na mchana kuwa usiku,

ambaye huyaita maji ya bahari

na kuyamwaga juu ya uso wa nchi:

Bwanandilo jina lake;

9 yeye hufanya maangamizo kwenye ngome

na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa),

10 mnamchukia yule akemeaye mahakamani,

na kumdharau yule ambaye husema kweli.

11 Mnamgandamiza maskini

na kumlazimisha awape nafaka.

Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,

hamtaishi ndani yake;

ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,

hamtakunywa divai yake.

12 Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu

na ukubwa wa dhambi zenu.

Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa

na kuzuia haki ya maskini mahakamani.

13 Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya

nyakati kama hizo,

kwa kuwa nyakati ni mbaya.

14 Tafuteni mema, wala si mabaya,

ili mpate kuishi.

NdipoBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote

atakuwa pamoja nanyi,

kama msemavyo yupo nanyi.

15 Yachukieni maovu, yapendeni mema;

dumisheni haki mahakamani.

YamkiniBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote

atawahurumia mabaki ya Yosefu.

16 Kwa hiyo hili ndilo Bwana,BwanaMungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo:

“Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote

na vilio vya uchungu

mahali pa njia kuu.

Wakulima wataitwa kuja kulia

na waombolezaji waje kuomboleza.

17 Kutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu,

kwa kuwa nitapita katikati yenu,”

asemaBwana.

Siku Ya Bwana

18 Ole wenu ninyi mnaoitamani

siku yaBwana!

Kwa nini mnaitamani siku yaBwana?

Siku hiyo itakuwa giza, si nuru.

19 Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba

kumbe akakutana na dubu,

kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake

na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta

kumbe akaumwa na nyoka.

20 Je, siku yaBwanahaitakuwa giza, na si nuru:

giza nene, bila mwonzi wa mwanga?

21 “Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini;

siwezi kuvumilia makusanyiko yenu.

22 Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa

na sadaka za nafaka,

sitazikubali.

Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani,

sitazitambua.

23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu!

Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

24 Lakini acheni haki itiririke kama mto,

na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!

25 “Je, mliniletea dhabihu na sadaka

mlipokuwa jangwani miaka arobaini,

Ee nyumba ya Israeli?

26 Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu:

Sikuthi mungu wenu mtawala,

Kiuni mungu wenu wa nyota;

ambao mliwatengeneza wenyewe.

27 Kwa sababu hiyo nitawapelekeni

uhamishoni mbali kupita Dameski,”

asemaBwana, ambaye jina lake

ni Mungu Mwenye Nguvu Zote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/AMO/5-ee752d29b5071367ece5f6ff3b14473b.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

6 + seven =