Habakuki 2

1 Nitasimama katika zamu yangu

na kujiweka mwenyewe juu ya maboma;

nitatazama nione atakaloniambia,

na ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili.

Jibu La Bwana

2 KishaBwanaakajibu:

“Andika ufunuo huu

na ukaufanye wazi juu ya vibao

ili mpiga mbiu akimbie nao.

3 Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika;

unazungumzia mambo ya mwisho

na kamwe hautakosea.

Iwapo utakawia, wewe usubiri;

kwa hakika utakuja na hautachelewa.

4 “Tazama, amejaa majivuno,

anavyovitamani si vya unyofu.

Lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake:

5 hakika mvinyo humsaliti;

ni mwenye kiburi na hana amani.

Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu

na kama kifo kamwe hatosheki;

anajikusanyia mataifa yote

na kuchukua watu wote mateka.

6 “Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema,

“ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa

na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu!

Ataendelea hivi kwa muda gani?’

7 Je, wadai wako hawatainuka ghafula?

Je, hawataamka na kukufanya utetemeke?

Kisha utakuwa mhanga kwao.

8 Kwa kuwa umeteka nyara mataifa mengi,

watu waliobaki watakuteka nyara wewe.

Kwa kuwa umemwaga damu ya mtu;

umeharibu nchi na miji

na kila mmoja ndani yake.

9 “Ole wake yeye ajengaye milki yake kwa mapato ya udhalimu,

awekaye kiota chake juu,

ili kukimbia makucha ya uharibifu!

10 Umefanya shauri la maangamizi ya watu wengi,

ukiaibisha nyumba yako mwenyewe

na kupotewa na maisha yako.

11 Mawe ya kuta yatapiga kelele,

na mihimili ya kazi ya mbao

itarudisha mwangwi wake.

12 “Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga

damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!

13 Je,BwanaMwenye Nguvu Zote hakuonyesha

kwamba kazi ya wanadamu

ni mafuta tu kwa ajili ya moto,

na kwamba mataifa

yanajichosha bure?

14 Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu waBwana,

kama maji yaifunikavyo bahari.

15 “Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo,

akiimimina kutoka kwenye kiriba

cha mvinyo mpaka wamelewa,

ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.

16 Utajazwa na aibu badala ya utukufu.

Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue!

Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume waBwanakinakujia,

na aibu itafunika utukufu wako.

17 Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika,

na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha.

Kwa sababu umemwaga damu ya mtu,

umeharibu nchi na miji

na kila mmoja aliyeko ndani yake.

18 “Sanamu ina thamani gani,

kwani mwanadamu ndiye aliyechonga?

Ama kinyago kinachofundisha uongo?

Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza

hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe;

hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.

19 Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’

Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’

Je, linaweza kuongoza?

Limefunikwa kwa dhahabu na fedha,

hakuna pumzi ndani yake.

20 LakiniBwanayuko katika Hekalu lake takatifu;

dunia yote na inyamaze mbele yake.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/HAB/2-04979c73066568b41ab1d6b764839675.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nineteen − ten =