Isaya 27

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

1 Katika siku ile,

Bwanaataadhibu kwa upanga wake,

upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,

# ataadhibu Lewiathaniyule nyoka apitaye mbio kwa mwendo laini,

Lewiathani yule nyoka mwenye kupindapinda;

atamwua joka huyo mkubwa sana wa baharini.

2 Katika siku ile:

“Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

3 Mimi,Bwana, ninalitunza,

nitalinyweshea maji mfululizo.

Ninalichunga mchana na usiku ili mtu ye yote asije akalidhuru.

4 Mimi sijakasirika.

Hata kama pangekuwepo michongoma

na miiba inayonikabili!

Ningepambana dhidi yake katika vita,

ningeliichoma moto yote.

5 Au niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,

wao na wafanye amani nami,

naam, wafanye amani nami.”

6 Katika siku zijazo Yakobo atatia mizizi,

Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,

naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.

7 Je,Bwanaamempiga kama alivyowapiga wale waliompiga?

Je, yeye ameuawa

kama wale waliouawa

ambao walimwua yeye?

8 Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye,

kwa mshindo wake mkali anamfukuza,

kama siku uvumapo upepo wa mashariki.

9 Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,

hili litakuwa ndiyo matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:

Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu

kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,

hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia

uvumba zitakazobaki zimesimama.

10 Mji ulio na boma umebaki ukiwa,

makao yaliyotelekezwa yameachwa kama jangwa,

huko ndama hulisha,

huko hujilaza,

wanakwanyua matawi yake.

11 Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa

nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.

Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,

kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,

Muumba wao hawaonyeshi fadhili.

12 Katika siku ileBwanaatapura kutoka matiririko ya mto wa Eufrati hadi Kijito cha Misri, nanyi, Ee Waisraeli mtakusanywa pamoja mmoja mmoja.

13 Katika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabuduBwanakatika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/27-11d9a8e1a22a0bf89939a171a02d608c.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ten − six =