Isaya 4

1 Katika siku ile wanawake saba

watamshika mwanaume mmoja

wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe

na kuvaa nguo zetu wenyewe,

ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako.

Utuondolee aibu yetu!”

Tawi La Bwana

2 Katika siku ile Tawi laBwanalitakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika.

3 Wale watakaoachwa Sayuni, watakaobaki Yerusalemu, wataitwa watakatifu, wale wote ambao wameorodheshwa miongoni mwa walio hai huko Yerusalemu.

4 Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto.

5 KishaBwanaataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana na kung’aa kwa miali ya moto wakati wa usiku, juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.

6 Utakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/4-29a0f8ff5e4f3c8fcfb5d73edd660c18.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ten − three =