Kutoka 27

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake ni dhiraa tatu;itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tanona upana wake dhiraa tano.

2 Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili kwamba zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana na uifunike madhabahu kwa shaba.

3 Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, sepeto zake, mabakuli ya kunyunyizia, nyuma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.

4 Kisha itengenezee hiyo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila pembe nne za huo wavu.

5 Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufike nusu ya kimo cha madhabahu.

6 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, ifunike kwa shaba.

7 Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe katika pande mbili za madhabahu, wakati inapobebwa.

8 Tengeneza madhabahu iwe na uvungu ndani yake, ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.

Ua Wa Kukutania

9 “Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,na itakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,

10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini. Pia kutakuwa na kulabu za fedha na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

11 Upande wa kaskazini itakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia na nguzo zake ishirini, na vitako ishirini vya shaba, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12 “Upande wa magharibi wa ua wa kukutania utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,nao utakuwa na mapazia na nguzo zake kumi na vitako vyake kumi.

13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakotokea, ua wa mkutano utakuwa na upana wa dhiraa hamsini.

14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano ambayo yatakuwa upande mmoja wa lango, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu,

15 Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tanokwa upande mwingine wa mlango, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.

16 “Kuhusu lango la kuingilia kwenye ua wa kukutania, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini, la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.

17 Nguzo zote zinazozunguka ua wa kukutania zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba.

18 Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba.

19 Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika Maskani kwa shughuli yo yote, pamoja na vigingi vyote, na hata vile vya ua wa kukutania vitakuwa vya shaba.

Mafuta Ya Kinara Cha Taa

20 “Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake daima.

21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele zaBwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/27-1a7f7488fcb35d2931e7edc419f53690.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − eight =