Mika 4

Mlima Wa Bwana

1 Katika siku za mwisho

mlima wa Hekalu laBwanautaimarishwa

na kuwa mkuu kuliko milima yote;

utainuliwa juu ya vilima

na mataifa yatamiminika humo.

2 Mataifa mengi yatakuja na kusema,

“Njoni, twendeni mlimani kwaBwana,

kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.

Atatufundisha njia zake,

ili tutembee katika mapito yake.”

Sheria itatoka Sayuni,

neno laBwanalitatoka Yerusalemu.

3 Atahukumu kati ya mataifa mengi

na ataamua migogoro ya mataifa

yenye nguvu na yaliyo mbali.

Watafua panga zao ziwe majembe ya kulimia

na mikuki yao kuwa miundu ya kukatia matawi.

Taifa halitachukua upanga dhidi ya taifa,

wala hawatajifunza vita tena.

4 Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake

na chini ya mtini wake,

wala hakuna mtu atakayewaogopesha,

kwa kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote amesema.

5 Mataifa yote yanaweza kutembea

katika jina la miungu yao;

sisi tutatembea katika jina laBwana

Mungu wetu milele na milele.

Mpango Wa Bwana

6 “Katika siku hiyo,” asemaBwana,

“nitawakusanya walemavu;

nitawakusanya walio uhamishoni

na wale niliowahuzunisha.

7 Nitawafanya walemavu kuwa mabaki,

wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu.

Bwanaatatawala juu yao katika Mlima Sayuni

kuanzia siku hiyo na hata milele.

8 Lakini kuhusu wewe, Ee mnara wa ulinzi wa kundi,

Ee ngome ya Binti Sayuni,

milki ya awali itarudishwa kwako,

ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”

9 Kwa nini sasa unalia kwa nguvu:

kwani huna mfalme?

Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate

kama ya mwanamke

aliye na utungu wa kuzaa?

10 Gaagaa kwa utungu, Ee Binti Sayuni,

kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa,

kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji

ukapige kambi uwanjani.

Utakwenda Babeli;

huko utaokolewa.

HukoBwanaatakukomboa

kutoka mikononi mwa adui zako.

11 Lakini sasa mataifa mengi

yamekusanyika dhidi yako.

Wanasema, “Mwache anajisiwe,

macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!”

12 Lakini hawayajui

mawazo yaBwana;

hawauelewi mpango wake,

yeye awakusanyaye kama miganda

kwenye sakafu ya kupuria.

13 “Inuka upure, Ee Binti Sayuni,

kwa kuwa nitakupa pembe za chuma;

nitakupa kwato za shaba

na utavunja vipande vipande mataifa mengi.”

Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwaBwana,

utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MIC/4-afe6010954f60b8538d4c7d5d9bcb9dc.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 + one =