Mika 5

Mtawala Aliyeahidiwa Kutoka Bethlehemu

1 Panga majeshi yako, Ee mji wa majeshi,

kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu.

Watampiga mtawala wa Israeli

shavuni kwa fimbo.

2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi,

ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda,

kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu

yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli,

ambaye asili yake ni kutoka zamani,

kutoka milele.”

3 Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati

mwanamke aliye na utungu atakapozaa

na ndugu zake wengine warudi

kujiunga na Waisraeli.

4 Atasimama na kulichunga kundi lake

katika nguvu yaBwana,

katika utukufu wa jina laBwanaMungu wake.

Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo

ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.

5 Naye atakuwa amani yao.

Ukombozi Na Uharibifu

Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu

na kupita katika ngome zetu,

tutawainua wachungaji saba dhidi yake,

hata viongozi wanane wa watu.

6 Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga,

nchi ya Nimrodi kwa upanga.

Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru

atakapoivamia nchi yetu

na kuingia katika mipaka yetu.

7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa

katikati ya mataifa mengi

kama umande kutoka kwaBwana,

kama manyunyu juu ya majani,

ambayo hayamngoji mtu

wala kukawia kwa mwanadamu.

8 Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa,

katikati ya mataifa mengi,

kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni,

kama mwana simba miongoni

mwa makundi ya kondoo,

ambaye anaumiza vibaya na kuwararua

kila anapopita katikati yao,

wala hakuna awezaye kuokoa.

9 Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako,

nao adui zako wote wataangamizwa.

10 “Katika siku ile,” asemaBwana,

“nitaangamiza farasi zenu katikati yenu

na kubomoa magari yenu ya vita.

11 Nitaiangamiza miji ya nchi yenu

na kuziangusha chini ngome zenu zote.

12 Nitaangamiza uchawi wenu

na hamtapiga tena ramli.

13 Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga

na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu;

hamtasujudia tena

kazi ya mikono yenu.

14 Nitang’oa nguzo za Ashera katikati yenu

na kubomoa miji yenu.

15 Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu

juu ya mataifa ambayo hayajanitii.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MIC/5-89f2f5314d9cbc53b197da6836b87709.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen − three =