Mika 6

Shauri La Bwana Dhidi Ya Israeli

1 Sikiliza asemaloBwana:

“Simama, tetea shauri lako mbele ya milima;

vilima na visikie lile unalotaka kusema.

2 Sikilizeni, Ee milima, mashtaka yaBwana,

sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia.

Kwa kuwaBwanaana shauri dhidi ya watu wake;

anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.

3 “Watu wangu, nimewatendea nini?

Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu.

4 Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa

kutoka nchi ya utumwa.

Nilimtuma Mose awaongoze,

pia Aroni na Miriamu.

5 Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu

alivyofanya shauri

na kile Balamu mwana wa Beori alichojibu.

Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali,

ili mfahamu matendo ya haki yaBwana.”

6 NimjieBwanana kitu gani na kusujudu

mbele za Mungu aliyetukuka?

Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa,

nije na ndama za mwaka mmoja?

7 Je,Bwanaatafurahishwa na kondoo dume elfu,

au mito elfu kumi ya mafuta?

Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu,

mtoto wangu mwenyewe

kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?

8 Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu.

Bwanaanataka nini kwako?

Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,

na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

Hatia Na Adhabu Ya Israeli

9 Sikiliza!Bwanaanauita mji:

kulicha jina lako ni hekima:

“Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru.

10 Je, bado nisahau, Ee nyumba ya uovu,

hazina yako uliyopata kwa udanganyifu

na vipimo vilivyopunguka,

ambavyo vimelaaniwa?

11 Je, naweza kuhukumu kuwa

mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia,

aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo?

12 Matajiri wake ni wajeuri;

watu wake ni waongo

na ndimi zao zinazungumza

kwa udanganyifu.

13 Kwa hiyo, nimeanza kukuharibu,

kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu.

14 Mtakula lakini hamtashiba;

matumbo yenu bado yatakuwa matupu.

Mtaweka akiba lakini hamtaokoa cho chote,

kwa sababu mtakachoweka akiba

nitatoa kwa upanga.

15 Mtapanda lakini hamtavuna;

mtakamua zeituni lakini

hamtatumia mafuta yake.

Mtakamua zabibu

lakini hamtakunywa hiyo divai.

16 Mmezishika sheria za Omri

na matendo yote ya nyumba ya Ahabu,

tena umefuata desturi zao.

Kwa hiyo nitakutoa kwa maangamizi

na watu wako kuwa dhihaka;

mtachukua dharau za mataifa.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MIC/6-ff861ca39e31ef65682dde44fedc0dd1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − 4 =