Yeremia 20

Yeremia Ateswa Na Pashuri

1 Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu laBwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya,

2 akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa katika mkatale katika Lango la Juu la Benyamini katika Hekalu laBwana.

3 Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwanahakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.

4 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Wayahudi wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli ama awaue kwa upanga.

5 Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao, yaani, mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.

6 Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”

Malalamiko Ya Yeremia

7 EeBwana, umenidanganya,

nami nikadanganyika;

wewe una nguvu kuliko mimi,

nawe umenishinda.

Ninadharauliwa mchana kutwa,

kila mmoja ananidhihaki.

8 Kila ninenapo, ninapiga kelele

nikitangaza ukatili na uharibifu.

Kwa hiyo neno laBwanalimeniletea matukano

na mashutumu mchana kutwa.

9 Lakini kama nikisema, “Sitamtaja

wala kusema tena kwa jina lake,”

neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,

moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.

Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;

kweli, siwezi kujizuia.

10 Ninasikia minong’ono mingi,

“Hofu iko pande zote!

Mshitakini! Twendeni tumshitaki!”

Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,

wakisema,

“Labda atadanganyika;

kisha tutamshinda

na kulipiza kisasi juu yake.”

11 LakiniBwanayu pamoja nami

kama shujaa mwenye nguvu;

hivyo washitaki wangu watajikwaa

na kamwe hawatashinda.

Watashindwa, nao wataaibika kabisa;

kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

12 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,

wewe umjaribuye mwenye haki

na kupima moyo na nia,

na nione ukilipiza kisasi juu yao,

kwa maana kwako

nimeliweka shauri langu.

13 MwimbieniBwana!

MpeniBwanasifa!

Huokoa uhai wa mhitaji

kutoka mikononi mwa waovu.

14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

Nayo isibarikiwe ile siku

mama yangu aliyonizaa!

15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

“Mtoto amezaliwa kwako,

tena mtoto wa kiume!”

16 Mtu huyo na awe kama miji ile

ambayoBwanaMungu

aliiangamiza bila huruma.

Yeye na asikie maombolezo asubuhi

na kilio cha vita wakati wa adhuhuri.

17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

nalo tumbo lake la uzazi

lingebaki kuwa kubwa daima.

18 Kwa nini basi nilitoka tumboni

ili kuona taabu na huzuni

na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/20-cedf2c89bb12c3fc49c923a2d0582c7b.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × four =