Yoeli 2

Jeshi La Nzige

1 Pigeni tarumbeta katika Sayuni;

pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu.

Wote waishio katika nchi na watetemeke,

kwa kuwa siku yaBwanainakuja. Iko karibu,

2 siku ya giza na huzuni,

siku ya mawingu na utusitusi.

Kama mapambazuko yasambaavyo

toka upande huu wa milima

hata upande mwingine

jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja.

Jambo kama hili halijakuwapo tangu zamani

wala halitakuwapo tena kamwe

kwa vizazi vijavyo.

3 Mbele yao moto unateketeza,

nyuma yao miali ya moto

inawaka kwa nguvu.

Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni,

nyuma yao ni jangwa lisilofaa:

hakuna kitu kinachowaepuka.

4 Wanaonekana kama farasi;

wanakwenda mbio

kama askari wapanda farasi.

5 Wanatoa sauti kama magari ya vita,

wanaporukaruka juu ya vilele vya milima,

kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua,

kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita.

6 Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu;

kila uso unabadilika rangi.

7 Wanashambulia kama wapiganaji wa vita;

wanapanda kuta kama askari.

Wote wanatembea katika safu,

hawapotoshi safu zao.

8 Hakuna anayemsukuma mwenzake;

kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.

Wanapita katika vizuizi

bila kuharibu safu zao.

9 Wanaenda kasi kuingia mjini;

wanakimbia ukutani.

Wanaingia ndani ya nyumba;

kwa kuingilia madirishani kama wevi.

10 Mbele yao dunia inatikisika,

anga linatetemeka,

jua na mwezi vinatiwa giza,

na nyota hazitoi mwanga wake tena.

11 Bwanaanatoa mshindo wa ngurumo

mbele ya jeshi lake;

majeshi yake hayana idadi,

ni wenye nguvu nyingi

wale ambao hutii agizo lake.

Siku yaBwanani kuu,

ni ya kutisha.

Ni nani anayeweza kuistahimili?

Rarueni Mioyo Yenu

12 “Hata sasa,” asemaBwana,

“nirudieni kwa mioyo yenu yote,

kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.”

13 Rarueni mioyo yenu

na siyo mavazi yenu.

MrudieniBwana, Mungu wenu,

kwa maana yeye ndiye mwenye neema

na mwingi wa huruma,

si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,

huona huruma, hujizuia kuleta maafa.

14 Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma

na kuacha baraka nyuma yake:

sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji

kwa ajili yaBwanaMungu wenu.

15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni,

tangazeni saumu takatifu,

liiteni kusanyiko takatifu.

16 Wakusanyeni watu,

wekeni wakfu kusanyiko;

waleteni pamoja wazee,

wakusanyeni watoto,

wale wanyonyao maziwa.

Bwana arusi na atoke chumbani mwake

na bibi arusi naye atoke katika chumba chake.

17 Makuhani, ambao wanahudumu mbele zaBwana,

na walie katikati ya ukumbi

wa Hekalu na madhabahu.

Waseme, “Wahurumie watu wako, EeBwana.

Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa,

neno la dhihaka kati ya mataifa.

Kwa nini wasemezane miongoni mwao,

‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”

Jibu La Bwana

18 KishaBwanaatakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake

na kuwa na huruma juu ya watu wake.

19 Bwanaatawajibu:

“Ninawapelekea nafaka,

mvinyo mpya na mafuta,

vya kuwatosha ninyi

hadi mridhike kabisa;

kamwe sitawafanya tena

kitu cha kudharauliwa na mataifa.

20 “Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi,

nikilisukuma ndani ya jangwa,

askari wa safu za mbele wakienda

ndani ya bahari ya mashariki

na wale wa safu za nyuma

katika bahari ya magharibi.

Uvundo wake utapaa juu;

harufu yake itapanda juu.”

Hakika ametenda mambo makubwa.

21 Usiogope, Ee nchi;

furahi na kushangilia.

HakikaBwanaametenda mambo makubwa.

22 Msiogope, Enyi wanyama pori,

kwa kuwa mbuga za malisho yenu

zinarudia ubichi.

Miti nayo inazaa matunda,

mtini na mzabibu inatoa utajiri wake.

23 Furahini, Enyi watu wa Sayuni,

shangilieni katikaBwanaMungu wenu,

kwa kuwa amewapa mvua za vuli

kwa kipimo cha haki.

Anawapelekea mvua nyingi,

mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.

24 Sakafu za kupuria zitajaa nafaka,

mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta.

25 “Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige:

parare, madumadu na tunutu,

jeshi langu kubwa ambalo

nililituma katikati yenu.

26 Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe,

na mtalisifu jina laBwanaMungu wenu,

ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu;

kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.

27 Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli

kwamba mimi ndimiBwanaMungu wenu,

na kwamba hakuna mwingine;

kamwe watu wangu hawataaibika tena.

Siku Ya Bwana

28 “Hata itakuwa, baada ya hayo,

nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu, waume kwa wake, watatabiri,

wazee wenu wataota ndoto,

na vijana wenu wataona maono.

29 Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho yangu.

30 Nami nitaonyesha maajabu katika mbingu

na juu ya nchi,

damu, moto na wimbi la moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza

na mwezi kuwa damu

kabla ya kuja siku yaBwana

iliyo kuu na ya kutisha.

32 Na kila mmoja atakayeliitia

jina laBwanaataokolewa.

Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu

kutakuwako wokovu,

kamaBwanaalivyosema,

miongoni mwa walionusurika

ambaoBwanaawaita.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOL/2-834e1ac8d2542f5b1a07a9f9571d5538.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eight + 20 =