Zaburi 144

Mfalme Amshukuru Mungu Kwa Ushindi

(Zaburi Ya Daudi)

1 Sifa ni kwaBwanaMwamba wangu,

aifundishaye mikono yangu vita,

vidole vyangu kupigana.

2 Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

ngao yangu ninayemkimbilia,

ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.

3 EeBwana, mwanadamu ni nini hata umjali,

Binadamu ni nini hata umfikirie?

4 Mwanadamu ni kama pumzi,

siku zake ni kama kivuli kinachopita.

5 EeBwana, pasua mbingu zako, ushuke,

gusa milima ili itoe moshi.

6 Peleka umeme wa radi na uwatawanye adui,

lenga mishale yako uwashinde.

7 Nyosha mkono wako kutoka juu,

nikomboe na kuniokoa kutoka katika maji makuu,

kutoka katika mikono ya wageni

8 ambao vinywa vyao vimejaa uongo,

mikono yao ya kuume ni midanganyifu.

9 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,

kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,

10 kwa Mmoja awapaye wafalme ushindi,

ambaye humwokoa Daudi,

mtumishi wake na upanga hatari.

11 Nikomboe na uniokoe

kutoka mikononi mwa wageni

ambao midomo yao imejaa uongo,

na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.

12 Kisha wana wetu wakati wa ujana wao

watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,

binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa

kuremba jumba la kifalme.

13 Ghala zetu zitajazwa

aina zote za mahitaji.

Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,

kwa makumi ya maelfu

katika mashamba yetu;

14 maksai wetu watakokota

mizigo mizito.

Hakutakuwa na kubomoka kuta,

hakuna kuchukuliwa mateka,

wala kilio cha taabu

katika barabara zetu.

15 Heri watu ambao hili ni kweli;

heri wale ambaoBwanani Mungu wao.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/144-86d8063c5d30fe1a92aca97c91b2c345.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − 7 =