Zaburi 145

Wimbo Wa Kusifu Ukuu Na Wema Wa Mungu

(Wimbo Wa Sifa. Wa Daudi)

1 Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme,

nitalisifu jina lako milele na milele.

2 Kila siku nitakusifu

na kulitukuza jina lako milele na milele.

3 Bwanani mkuu, anayestahili kusifiwa sana,

ukuu wake haupimiki.

4 Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine,

watasimulia matendo yako makuu.

5 Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako,

nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.

6 Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha,

nami nitatangaza matendo yako makuu.

7 Wataadhimisha wema wako mwingi

na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.

8 Bwanani mwenye neema na mwingi wa huruma,

si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo.

9 Bwanani mwema kwa wote,

ana huruma kwa vyote alivyovifanya.

10 EeBwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu,

watakatifu wako watakutukuza.

11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako

na kusema juu ya ukuu wako,

12 ili watu wote wajue matendo yako makuu

na utukufu wa fahari ya ufalme wako.

13 Ufalme wako ni ufalme wa milele,

mamlaka yako hudumu vizazi vyote.

Bwanani mwaminifu kwa ahadi zake zote

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

14 Bwanahuwategemeza wote waangukao

na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.

15 Macho yao wote yanakutazama wewe,

nawe huwapa chakula chao wakati wake.

16 Waufumbua mkono wako,

watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

17 Bwanani mwenye haki katika njia zake zote

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

18 Bwanayu karibu na wote wamwitao,

karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

19 Huwatimizia wamchao matakwa yao,

husikia kilio chao na kuwaokoa.

20 Bwanahuwalinda wote wampendao,

bali waovu wote atawaangamiza.

21 Kinywa changu kitazinena sifa zaBwana.

Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu

milele na milele.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/145-926e00a6b42abbd14c4a202c1b1131c0.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 + ten =