Zaburi 147

Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote

1 MsifuniBwana.

Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,

jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!

2 Bwanahujenga Yerusalemu,

huwakusanya Israeli walio uhamishoni.

3 Anawaponya waliovunjika mioyo

na kuvifunga vidonda vyao.

4 Huzihesabu nyota

na huipa kila moja jina lake.

5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,

ufahamu wake hauna kikomo.

6 Bwanahuwahifadhi wanyenyekevu

lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.

7 MwimbieniBwanakwa shukrani,

mpigieni Mungu wetu kinubi.

8 Yeye huzifunika anga kwa mawingu,

huinyeshea ardhi mvua

na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.

9 Huwapa mifugo chakula

na makinda ya kunguru yanapolia.

10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi,

wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu,

11 Bwanahupendezwa na wale wamchao,

wale wanaoweka tumaini lao

katika upendo wake usiokoma.

12 MtukuzeBwana, Ee Yerusalemu,

msifu Mungu wako, Ee Sayuni,

13 kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako

na huwabariki watu wako walio ndani yako.

14 Huwapa amani mipakani mwenu

na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.

15 Hutuma amri yake duniani,

neno lake hukimbia kasi.

16 Anatandaza theluji kama sufu

na kutawanya umande kama majivu.

17 Huvurumisha mvua yake ya mawe

kama changarawe.

Ni nani awezaye kustahimili

ukali wa baridi yake?

18 Hutuma neno lake na kuviyeyusha,

huvumisha upepo wake,

maji hutiririka.

19 Amemfunulia Yakobo neno lake,

sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

20 Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lo lote,

hawazijui sheria zake.

MsifuniBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/147-6ec7e09cc3e3b2da07364666932b199b.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 + 2 =