Zaburi 148

Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu

1 MsifuniBwana.

MsifuniBwanakutoka mbinguni,

msifuni juu vileleni.

2 Msifuni, enyi malaika wake wote,

msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,

msifuni yeye, enyi nyota zote zing’aazo.

4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana

na ninyi maji juu ya anga.

5 Vilisifu jina laBwana

kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

6 Aliviweka mahali pake milele na milele,

alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

7 MtukuzeniBwanakutoka duniani,

ninyi viumbe vikubwa vya baharini

na vilindi vyote vya bahari,

8 umeme wa radi na mvua ya mawe,

theluji na mawingu,

pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,

9 ninyi milima na vilima vyote,

miti ya matunda na mierezi yote,

10 wanyama wa mwituni na mifugo yote,

viumbe vidogo na ndege warukao,

11 wafalme wa dunia na mataifa yote,

ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,

12 wanaume vijana na wanawali,

wazee na watoto.

13 Wote na walisifu jina laBwana,

kwa maana jina lake pekee limetukuka,

utukufu U juu ya nchi na mbingu.

14 Amewainulia watu wake pembe,

sifa ya watakatifu wake wote,

ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.

MsifuniBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/148-41b131ad3ce27044f048b5cc8f4781ee.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 − 12 =