Zaburi 21

Shukrani kwa Mungu Kwa Ajili Ya Ushindi

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

1 EeBwana, mfalme huzifurahia nguvu zako.

Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake

kwa ushindi unaompa!

2 Umempa haja ya moyo wake

na hukumzuilia maombi ya midomo yake.

3 Ulimkaribisha kwa baraka tele

na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

4 Alikuomba maisha, nawe ukampa,

wingi wa siku milele na milele.

5 Kutokana na ushindi uliompa,

utukufu wake ni mkubwa,

umeweka juu yake fahari na utukufu.

6 Hakika umempa baraka za milele,

umemfanya awe na furaha

kwa shangwe ya uwepo wako.

7 Kwa kuwa mfalme anamtumainiBwana;

kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

8 Mkono wako utawashika adui zako wote,

mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.

9 Wakati utakapojitokeza utawafanya

kama tanuru ya moto.

Katika ghadhabu yakeBwanaatawameza,

moto wake utawateketeza.

10 Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani,

uzao wao kutoka katika wanadamu.

11 Ingawa watapanga mabaya dhidi yako

na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,

12 kwa kuwa utawafanya wakimbie

utakapowalenga usoni pao

kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.

13 EeBwana, utukuzwe katika nguvu zako,

tutaimba na kusifu nguvu zako.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/21-d146c2180055da91be31c243779ac087.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − 9 =