Zaburi 22

Kilio Cha Uchungu Na Wimbo Wa Sifa

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Utenzi Wa Kulungu Wa Alfajiri)

1 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa?

Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?

2 Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu,

hata usiku, sinyamazi.

3 Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Mtakatifu;

# wewe ni sifa ya Israeli.

4 Katika wewe baba zetu waliweka tumaini lao,

walikutumaini nawe ukawaokoa.

5 Walikulilia wewe na ukawaokoa,

walikutegemea wewe nao hawakuaibika.

6 Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu,

wanaume wamenibeza

na watu wamenidharau

7 Wote wanionao hunidhihaki,

hunivurumishia matusi,

wakitikisa vichwa vyao:

8 Husema, “AnamtegemeaBwana,

basiBwanana amwokoe.

Amkomboe basi, kwa maana

anapendezwa naye.”

9 Hata hivyo ulinitoa tumboni,

ukanifanya nikutegemee

hata nilipokuwa ninanyonya

matiti ya mama yangu.

10 Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,

toka tumboni mwa mama yangu

umekuwa Mungu wangu.

11 Usiwe mbali nami,

kwa maana shida iko karibu

na hakuna wa kunisaidia.

12 Mafahali wengi wamenizunguka,

mafahali wa Bashani wenye nguvu

wamenizingira.

13 Simba wangurumao wanaorarua mawindo

yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.

14 Nimemiminwa kama maji,

mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake.

Moyo wangu umegeuka kuwa nta,

umeyeyuka ndani yangu.

15 Nguvu zangu zimekauka kama kigae,

ulimi wangu umegandamana

na kaakaa la kinywa changu,

kwa sababu umenilaza

katika mavumbi ya kifo.

16 Mbwa wamenizunguka,

kundi la watu waovu limenizingira,

wametoboa mikono yangu na miguu yangu.

17 Naweza kuhesabu mifupa yangu yote,

watu wananikodolea macho na kunisimanga.

18 Wanagawana mavazi yangu wao kwa wao

na nguo zangu wanazipigia kura.

19 Lakini wewe, EeBwana,

usiwe mbali,

Ee Nguvu yangu,

uje haraka unisaidie.

20 Okoa maisha yangu na upanga,

uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.

21 Niokoe kutoka kinywani mwa simba,

niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.

22 Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu,

katika kusanyiko nitakusifu wewe.

23 Ninyi ambao mnamchaBwanamsifuni!

Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo,

mheshimuni yeye!

Mcheni yeye, ninyi

wazao wote wa Israeli!

24 Kwa maana hakupuuza wala kudharau

mateso ya aliyeonewa;

hakumficha uso wake

bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.

25 Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu

katika kusanyiko kubwa,

nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe.

26 Maskini watakula na kushiba,

wale wamtafutaoBwanawatamsifu,

mioyo yenu na iishi milele!

27 Miisho yote ya dunia itakumbuka

na kumgeukiaBwana,

nazo jamaa zote za mataifa

watasujudu mbele zake,

28 kwa maana ufalme ni waBwana

naye hutawala juu ya mataifa.

29 Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu;

wote waendao mavumbini

watapiga magoti mbele yake,

wote ambao hawawezi

kudumisha uhai wao.

30 Wazao wa baadaye watamtumikia yeye;

vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.

31 Watatangaza haki yake kwa watu

ambao hawajazaliwa bado,

kwa maana yeye ametenda hili.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/22-c4299ee39d33f726a920e2bded588c50.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 − one =