Zaburi 3

Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada

(Zaburi Ya Daudi Alipomkimbia Absalomu)

1 EeBwana, tazama adui zangu walivyo wengi!

Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

2 Wengi wanasema juu yangu,

“Mungu hatamwokoa.”

3 Lakini wewe, EeBwana, ni ngao pande zote;

umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

4 NinamliliaBwanakwa sauti kuu,

naye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu.

5 Ninajilaza na kupata usingizi;

naamka tena, kwa maanaBwanahunitegemeza.

6 Sitaogopa makumi elfu ya adui,

wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

7 EeBwana, amka!

Uniokoe, Ee Mungu wangu!

Wapige adui zangu wote kwenye taya,

vunja meno ya waovu.

8 Kwa maana wokovu watoka kwaBwana.

Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/3-02ebf1108eb4cf43d48b6134dc9a3fcb.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × five =