Ayubu 11

Sofari Anasema: Hatia Ya Ayubu Inastahili Adhabu 1 Ndipo Sofari, Mnaamathi akajibu: 2 “Je, maneno haya yote yapite bila kujibiwa? Je, huyu mnenaji athibitishwe kuwa na haki? 3 Je, maneno yako ya upuzi yawafanye watu wanyamaze kimya? Je, mtu asikukemee unapofanya dhihaka? 4 Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili nami ni safi mbele zako.’ 5 […]

Ayubu 12

Ayubu Anajibu: Mimi Ni Mtu Wa Kuchekwa 1 Ndipo Ayubu akajibu: 2 “Bila shaka ninyi ndio watu, nayo hekima itakoma mtakapokufa! 3 Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi, Mimi si duni kwenu. Ni nani asiyejua mambo haya yote? 4 “Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu, mimi ni mtu wa […]

Ayubu 13

1 “Macho yangu yameona hili lote, masikio yangu yamesikia na kulielewa. 2 Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua, mimi si mtu duni kuliko ninyi. 3 Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu. 4 Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo, ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! 5 Laiti wote mngenyamaza kimya! […]

Ayubu 14

1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache nazo zimejaa taabu. 2 Huchanua kama ua kisha hunyauka, huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu. 3 Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? Je, utamleta mbele yako katika hukumu? 4 Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka katika kitu najisi? Hakuna awezaye! 5 Siku za […]

Ayubu 15

Elifazi Anaongea: Ayubu Anadhoofisha Imani 1 Kisha Elifazi, Mtemani akajibu: 2 “Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu, au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki? 3 Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, kwa hotuba zisizo na maana? 4 Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu na kuzuia ibada mbele za Mungu. […]

Ayubu 16

Ayubu Anathibitisha Tena Hali Yake Ya Kutokuwa Na Hatia 1 Kisha Ayubu akajibu: 2 “Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha! 3 Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? 4 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; […]

Ayubu 17

1 Moyo wangu umevunjika, siku zangu zimefupishwa, kaburi linaningojea. 2 Hakika wenye mizaha wamenizunguka, macho yangu yamebaki kutazama uadui wao. Ayubu Anaomba Msaada 3 “Ee Mungu, nipe dhamana unayodai. Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu? 4 Umezifunga akili zao zisipate ufahamu, kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi. 5 Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili […]

Ayubu 18

Bildadi Anasema: Mungu Huwaadhibu Waovu 1 Bildadi, Mshuhi akajibu: 2 “Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea. 3 Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama na kuonekana wajinga machoni pako? 4 Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni […]

Ayubu 19

Ayubu Anajibu: Najua Mkombozi Wangu Yu Hai 1 Ndipo Ayubu akajibu: 2 “Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini na kuniponda kwa maneno yenu? 3 Mara kumi hizi mmenishutumu, bila aibu mnanishambulia. 4 Kama ni kweli nimepotoka, kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe. 5 Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu na kwa kutumia unyonge wangu dhidi yangu, […]

Ayubu 20

Sofari Anasema: Uovu Hupokea Malipo Ya Haki 1 Ndipo Sofari, Mnaamathi akajibu na kusema: 2 “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, kwa sababu nimehangaika sana. 3 Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima, nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu. 4 “Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani, 5 macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, […]