Hesabu 21

Nchi Ya Aradi Yaangamizwa 1 Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyeishi huko Negebu aliposikia kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja kwa njia ya Atharimu, aliwashambulia Waisraeli na kuwateka baadhi yao. 2 Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwaBwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.” 3 Bwanaakasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya […]

Hesabu 22

Balaki Anamwita Balaamu 1 Kisha Waisraeli wakasafiri katika tambarare za Moabu na kupiga kambi kando ya Mto Yordani, ng’ambo ya Yeriko. 2 Basi Balaki mwana wa Sipori, aliona mambo yote yale Israeli aliyowatendea Waamori; 3 Moabu aliogopa, kwa kuwa walikuwapo watu wengi sana. Hakika, Moabu alijawa na hofu kubwa kwa sababu ya Waisraeli. 4 Wamoabu […]

Hesabu 23

Ujumbe Wa Kwanza Wa Balaamu 1 Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, mnitayarishie mafahali saba na kondoo waume saba.” 2 Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema; hao wawili kila mmoja wao akatoa fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu. 3 Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda […]

Hesabu 24

1 Basi Balaamu alipoona imempendezaBwanakubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani. 2 Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake, 3 naye akatoa ujumbe wake: “Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori, ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona […]

Hesabu 25

Moabu Yashawishi Israeli 1 Wakati Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Kimoabu, 2 ambao waliwaalika kushiriki katika kutoa kafara kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hii. 3 Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao. 4 Bwanaakamwambia Mose, “Uwachukue viongozi […]

Hesabu 26

Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili 1 Baada ya hiyo tauni,Bwanaakamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, 2 “Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.” 3 Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya […]

Hesabu 27

Binti Wa Selofehadi 1 Binti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yosefu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia 2 ingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Mose, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko […]

Hesabu 28

Sadaka Za Kila Siku 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ 3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtoleaBwana: wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama […]

Hesabu 29

Sikukuu Ya Tarumbeta 1 “ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. 2 Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayoBwanaya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. […]

Hesabu 30

Nadhiri 1 Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndiloBwanaanaloagiza: 2 Wakati mwanaume awekapo nadhiri kwaBwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema. 3 “Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwaBwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi, 4 na baba yake akasikia […]