Hesabu 11

Moto Kutoka Kwa Bwana 1 Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwaBwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwaBwanaukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. 2 Watu walipomlilia Mose, akamwombaBwana, nao moto ukazimika. 3 Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwaBwanauliwaka miongoni mwao. Kware […]

Hesabu 12

Miriamu Na Aroni Wampinga Mose 1 Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 2 Waliuliza, “Je,Bwanaamesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” NayeBwanaakasikia hili. 3 (Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine ye yote katika uso wa […]

Hesabu 13

Kupeleleza Kanaani 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka katika kila kabila la baba zao tuma mmoja wa viongozi wao.” 3 Hivyo kwa agizo laBwanaMose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. 4 Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana […]

Hesabu 14

Watu Wanaasi 1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 3 Kwa niniBwanaanatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na […]

Hesabu 15

Sadaka Za Nyongeza 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Baada ya ninyi kuingia katika nchi ninayowapa kama nyumbani, 3 nanyi mkitoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kutoka katika makundi ya ng’ombe au kondoo, kama harufu nzuri inayompendezaBwana, ikiwa ni sadaka za kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum ama sadaka ya hiari […]

Hesabu 16

Kora, Dathani Na Abiramu 1 Kora mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, pamoja na baadhi ya Wareubeni, yaani Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni mwana wa Palethi, wakachukua baadhi ya watu, 2 wakainuka dhidi ya Mose. Pamoja nao walikuwapo wanaume wa Kiisraeli 250, watu waliojulikana, viongozi wa jumuiya waliokuwa wameteuliwa […]

Hesabu 17

Kuchipuka Kwa Fimbo Ya Aroni 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Sema na Waisraeli, na ujipatie fimbo kumi na mbili kutoka kwao, moja kutoka kwa kila mmoja wa viongozi wa kabila za baba zao. Andika jina la kila mtu kwenye fimbo yake. 3 Kwenye fimbo ya Lawi andika jina la Aroni, kwa maana ni lazima iwepo fimbo […]

Hesabu 18

Wajibu Wa Makuhani Na Walawi 1 Bwanaakamwambia Aroni, “Wewe, wanao na jamaa ya baba yako mtawajibika kwa makosa dhidi ya mahali patakatifu, wewe na wanao peke yenu ndio mtakaowajibika kwa makosa dhidi ya ukuhani. 2 Walete Walawi wenzako kutoka kabila la baba zako ili waungane nanyi na kuwasaidia wakati wewe na wanao mnapohudumu mbele ya […]

Hesabu 19

Maji Ya Utakaso 1 Bwanaakamwambia Mose na Aroni: 2 “Hivi ndivyo sheria ambayoBwanaameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa na ambaye hajapata kufungwa nira. 3 Mpeni kuhani Eleazari huyo mtamba; naye atatolewa nje ya kambi na kuchinjwa mbele yake huyo kuhani. 4 Kisha kuhani Eleazari atachukua baadhi ya damu yake […]

Hesabu 20

Maji Kutoka Kwenye Mwamba 1 Katika mwezi wa kwanza jumuiya yote ya Kiisraeli ilifika kwenye Jangwa la Sini, nao wakakaa Kadeshi. Miriamu akafa huko na kuzikwa. 2 Mahali hapo hapakuwa na maji kwa ajili ya jumuiya hiyo, nao wakakusanyika ili kumpinga Mose na Aroni. 3 Watu wakagombana na Mose, na kusema, “Laiti tungelikufa wakati ndugu […]