Isaya 51

Wokovu Wa Milele Kwa Sayuni 1 “Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki na mnaomtafutaBwana: Tazameni katika mwamba ambako ndiko mlikokatwa na mahali pa kuvunjia mawe ambako ndiko mlikochongwa; 2 mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, ambaye ndiye aliyewazaa. Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu, nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi. 3 HakikaBwanaataifariji Sayuni naye atayaangalia kwa huruma magofu […]

Isaya 52

1 Amka, amka, Ee Sayuni, jivike nguvu. Vaa mavazi yako ya fahari, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu. Asiyetahiriwa na aliye najisi hataingia kwako tena. 2 Jikung’ute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, Ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako. Ee Binti Sayuni uliye mateka. 3 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana: “Mliuzwa pasipo malipo, nanyi […]

Isaya 53

1 Ni nani aliyeamini ujumbe wetu na mkono waBwana umefunuliwa kwa nani? 2 Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvuta kwake, hakuwa na cho chote katika kuonekana kwake cha kutufanya tumtamani. 3 Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso. […]

Isaya 54

Utukufu Wa Baadaye Wa Sayuni 1 “Imba, Ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, ninyi ambao kamwe hamkupata utungu wa kuzaa; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asemaBwana. 2 “Panua mahali pa hema lako, tandaza mapazia ya hema […]

Isaya 55

Mwaliko Kwa Wenye Kiu 1 “Njoni, ninyi nyote wenye kiu, njoni kwenye maji; nanyi ambao hamna fedha, njoni, nunueni na mle! Njoni, nunueni divai na maziwa bila fedha na bila gharama. 2 Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula, na kutaabikia kitu kisichoshibisha? Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri, nazo nafsi zenu […]

Isaya 56

Wokovu Kwa Ajili Ya Wengine 1 Hili ndilo asemaloBwana: “Dumisheni haki na mkatende lile lililo sawa, kwa maana wokovu wangu u karibu na haki yangu itafunuliwa upesi. 2 Amebarikiwa mtu yule atendaye hili, mtu yule alishikaye kwa uthabiti, yeye ashikaye Sabato bila kuinajisi, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.” 3 Usimwache mgeni aambatanaye naBwanaaseme, […]

Isaya 57

Ibada Ya Sanamu Ya Israeli Iliyo Batili 1 Mwenye haki hupotea, wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake; watu wanaomcha Mungu huondolewa, wala hakuna hata mmoja anayeelewa kuwa wenye haki wameondolewa wasipatikane na maovu. 2 Wale waendao kwa unyofu huwa na amani; hupata pumziko walalapo mautini. 3 “Lakini ninyi, njoni hapa, ninyi wana wa […]

Isaya 58

Mfungo Wa Kweli 1 “Piga kelele, usizuie. Paza sauti yako kama tarumbeta. Watangazieni watu wangu uasi wao na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao. 2 Kwa maana kila siku hunitafuta, wanaonekana kutaka kujua njia zangu, kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lile lililo sawa na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake. Hutaka kwangu maamuzi ya haki, […]

Isaya 59

Dhambi, Toba Na Ukombozi 1 Hakika mkono waBwanasi mfupi hata usiweze kuokoa, wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia. 2 Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili asisikie. 3 Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu na vidole vyenu kwa hatia. Midomo yenu imenena uongo, […]

Isaya 60

Utukufu Wa Sayuni 1 “Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu waBwanaumezuka juu yako. 2 Tazama, giza litaifunika dunia na giza kuu litayafunika mataifa, lakiniBwanaatazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako. 3 Mataifa wataijia nuru yako na wafalme kuujia mwanga wa mapambazuko yako. 4 “Inua macho yako na utazame pande zote: […]