Isaya 61

Mwaka Wa Upendeleo Wa Bwana 1 Roho waBwanaMwenyezi yu juu yangu, kwa sababuBwanaamenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao, 2 kutangaza mwaka waBwanauliokubaliwa na siku ya kisasi ya Mungu wetu, kuwafariji wote waombolezao, 3 na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, […]

Isaya 62

Jina Jipya La Sayuni 1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza kimya, kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, wokovu wake kama mwanga wa moto. 2 Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa chaBwanakitatamka. 3 Utakuwa taji ya fahari mkononi mwaBwana, […]

Isaya 63

Siku Ya Mungu Ya Kisasi Na Ukombozi 1 Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, mwenye nguvu wa kuokoa.” 2 Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo […]

Isaya 64

1 Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini, kwamba milima ingelitetemeka mbele zako! 2 Kama vile moto uteketezavyo vijiti na kusababisha maji kuchemka, shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako! 3 Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia, ulishuka nayo milima ikatetemeka mbele zako. 4 Tangu nyakati za […]

Isaya 65

Hukumu Na Wokovu 1 “Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia, nimeonekana kwa watu wale ambao hawakunitafuta. Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu, nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’ 2 Mchana kutwa nimeinyosha mikono yangu kwa watu wakaidi, wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, wafuatao mawazo yao wenyewe, 3 taifa ambalo daima hunikasirisha machoni pangu, wakitoa […]

Isaya 66

Hukumu Na Matumaini 1 Hili ndilo asemaloBwana, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Iko wapi nyumba mtakayojenga kwa ajili yangu? Mahali pangu pa kupumzika patakuwa wapi? 2 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asemaBwana. “Mtu huyu ndiye ninayemthamini: yeye ambaye ni mnyenyekevu na […]