Isaya 41

Msaidizi Wa Israeli 1 “Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa! Mataifa na wafanye upya nguvu zao! Wao na wajitokeze, kisha waseme, tukutane pamoja mahali pa hukumu. 2 “Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki, akimwita katika haki kwa utumishi wake? Huyatia mataifa mikononi mwake na kuwatiisha wafalme mbele zake. Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake, huwafanya […]

Isaya 42

Mtumishi Wa Bwana 1 “Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa. 2 Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani. 3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja na utambi ufukao moshi hatauzima. Kwa uaminifu ataleta haki, 4 hatazimia roho wala kukata tamaa mpaka […]

Isaya 43

Mwokozi Pekee Wa Israeli 1 Lakini sasa hili ndilo asemaloBwana, yeye aliyekuumba, Ee Yakobo, yeye aliyekuhuluku, Ee Israeli: “Usiogope kwa maana nimekukomboa, nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu. 2 Unapopita kwenye maji makuu, nitakuwa pamoja nawe, unapopita katika mito ya maji, hayatakugharikisha. Utakapopita katika moto, hutaungua, miali ya moto haitakuunguza. 3 Kwa kuwa […]

Isaya 44

Israeli Aliyechaguliwa 1 “Lakini sasa sikiliza, Ee Yakobo, mtumishi wangu, Israeli, niliyemchagua. 2 Hili ndilo asemaloBwana, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, # Yeshuruni, niliyekuchagua. 3 Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka; nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako, […]

Isaya 45

Koreshi Chombo Cha Mungu 1 “Hili ndilo asemaloBwanakwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili kwamba malango yasije yakafungwa: 2 Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja malango ya shaba na kukatakata mapingo ya chuma. 3 Nitakupa hazina […]

Isaya 46

Miungu Ya Babeli 1 Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama; sanamu zao hubebwa na wanyama wa mizigo. Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, mzigo kwa waliochoka. 2 Vinyago pamoja na wale wanaovibeba wanainama chini; hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu, wote wanakwenda utumwani pamoja. 3 “Nisikilizeni mimi, Ee nyumba ya Yakobo, ninyi nyote […]

Isaya 47

Anguko La Babeli 1 “Shuka uketi mavumbini, Ee Bikira Binti Babeli; keti chini pasipo na kiti cha enzi, Ee binti wa Wakaldayo. Hutaitwa tena mwororo wala wa kupendeza. 2 Chukua mawe ya kusagia na usage unga, vua shela yako. Pandisha mavazi yako, ondoa viatu vyako, vuka vijito kwa shida. 3 Uchi wako utafunuliwa na aibu […]

Isaya 48

Israeli Mkaidi 1 “Sikilizeni hili, Ee nyumba ya Yakobo, ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, ninyi mnaoapa kwa jina laBwana, mnaomwomba Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli au kwa haki; 2 ninyi mnaojiita raia wa mji mtakatifu, na kumtegemea Mungu wa Israeli, BwanaMwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: […]

Isaya 49

Mtumishi Wa Bwana 1 Nisikilizeni, Enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwaBwanaaliniita, tangu kuzaliwa kwangu amelitaja jina langu. 2 Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa na kunificha katika podo lake. 3 Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika yeye nitaonyesha […]

Isaya 50

Dhambi Ya Israeli Na Utii Wa Mtumishi 1 Hili ndilo asemaloBwana: “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako ambayo kwayo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani miongoni mwa watu wanaonidai? Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, kwa sababu ya makosa mama yenu aliachwa. 2 Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja? Nilipoita, kwa nini […]