Isaya 31

Ole Wa Wale Wanaotegemea Misri 1 Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada, wale wategemeao farasi, wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita na katika nguvu nyingi za wapanda farasi, lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, wala hawatafuti msaada kwaBwana. 2 Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta […]

Isaya 32

Ufalme Wa Haki 1 Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu na watawala watatawala kwa haki. 2 Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo na kimbilio kutokana na dhoruba, kama vijito vya maji jangwani na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu. 3 Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena, nayo masikio ya […]

Isaya 33

Taabu Na Msaada 1 Ole wako wewe, Ee mharabu, wewe ambaye hukuharibiwa! Ole wako, Ee msaliti, wewe ambaye hukusalitiwa! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa; utakapokwisha kusaliti, utasalitiwa. 2 EeBwana, uturehemu, tunakutamani. Uwe nguvu yetu kila asubuhi na wokovu wetu wakati wa taabu. 3 Kwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia; unapoinuka, mataifa hutawanyika. 4 Mateka yako, Enyi […]

Isaya 34

Hukumu Dhidi Ya Mataifa 1 Njoni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize; sikilizeni kwa makini, enyi kabila za watu! Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake, ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake! 2 Bwanaameyakasirikia mataifa yote; ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. Atawaangamiza kabisa, atawatia mikononi mwa wachinjaji. 3 Waliouawa watatupwa nje, maiti […]

Isaya 35

Furaha Ya Waliokombolewa 1 Jangwa na nchi kame vitafurahi; nyika itashangilia na kuchanua maua. Kama waridi, 2 litachanua maua, litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha. Litapewa utukufu wa Lebanoni. Fahari ya Karmeli na Sharoni; wataona utukufu waBwana, fahari ya Mungu wetu. 3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea, 4 waambieni wale […]

Isaya 36

Senakeribu Anatishia Yerusalemu 1 Katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwa Mfalme Hezekia, Mfalme Senakeribu wa Ashuru alishambulia miji yote ya Yuda yenye maboma na kuiteka. 2 Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma Amirijeshi kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Amirijeshi aliposimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu […]

Isaya 37

Kuokolewa Kwa Yerusalemu Kunatabiriwa 1 Wakati Mfalme Hezekia aliposikia hili, alirarua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda hekaluni mwaBwana. 2 Akawatuma Eliakimu msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu na makuhani viongozi, wote wakiwa wamevaa nguo ya gunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi. 3 Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku […]

Isaya 38

Kuugua Kwa Mfalme Hezekia 1 Katika siku hizo Hezekia akaugua naye akawa karibu na kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kumwambia, “Hili ndilo asemaloBwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.” 2 Hezekia akageuza uso wake kuelekea ukutani na kumwombaBwana, 3 “EeBwana, kumbuka, jinsi nilivyotembea mbele zako kwa uaminifu na kujitoa […]

Isaya 39

Wajumbe Kutoka Babeli 1 Wakati huo Merodaki-Baladani mwana wa Baladani mfalme wa Babeli alimpelekea Hezekia barua na zawadi, kwa kuwa alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake. 2 Hezekia akawapokea wajumbe hao kwa furaha na kuwaonyesha kile kilichokuwa ndani ya ghala zake: Fedha, dhahabu, vikolezo, mafuta safi, silaha zake zote za vita na kila […]

Isaya 40

Faraja Kwa Watu Wa Mungu 1 Wafarijini, wafarijini watu wangu, asema Mungu wenu. 2 Sema na Yerusalemu kwa upole, umtangazie kwamba kazi yake ngumu imekamilika, kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia, kwamba amepokea kutoka mkononi mwaBwana maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote. 3 Sauti ya mtu aliaye: “Itengenezeni jangwani njia yaBwana, nyosheni njia kuu nyikani […]