Matendo 11

Petro Aeleza Alivyotumwa Kwa Watu Mataifa 1 Mitume na ndugu walioamini waliokuwa huko Uyahudi wakasikia kuwa watu Mataifa nao wamepokea neno la Mungu. 2 Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, wale wa tohara waliokuwa wameamini wakamshutumu, 3 wakisema, “Ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.” 4 Ndipo Petro akaanza kuwaeleza kuhusu mambo yote yalivyotokea hatua kwa […]

Matendo 12

Yakobo Auawa, Petro Atiwa Gerezani 1 Ilikuwa wakati kama huu Mfalme Herode Agripa aliwakamata baadhi ya watu wa kanisa. 2 Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. 3 Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. 4 Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya […]

Matendo 13

SAFARI YA KWANZA YA PAULO YA KITUME (13:1–14:28) Barnaba Na Sauli Wanatumwa 1 Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Luko Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa na Sauli. 2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi […]

Matendo 14

Paulo Na Barnaba Huko Ikonio 1 Huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi kama kawaida yao. Huko wakahubiri kwa uwezo mkubwa kiasi kwamba Wayahudi pamoja na watu Mataifa wakaamini. 2 Lakini wale Wayahudi waliokataa kuamini, wakawachochea watu Mataifa, wakatia chuki ndani ya mioyo yao dhidi ya wale walioamini. 3 Hivyo Paulo […]

Matendo 15

Baraza Huko Yerusalemu 1 Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha ndugu walioamini kwamba, “Isipokuwa mmetahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Mose, hamwezi kuokoka.” 2 Baada ya Paulo na Barnaba kutokukubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kuingia Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na […]

Matendo 16

Timotheo Aungana Na Paulo Na Sila 1 Paulo akafika Derbe na kisha Listra, ambako kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, ambaye mama yake alikuwa Myahudi aliyeamini, lakini baba yake alikuwa Myunani. 2 Alikuwa amesifiwa sana na wale ndugu waliokuwa wameamini huko Listra na Ikonio 3 Paulo alitaka Timotheo afuatane naye, hivyo akamchukua na kumtahiri […]

Matendo 17

Ghasia Huko Thesalonike 1 Wakasafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. 2 Kama desturi yake Paulo aliingia ndani ya sinagogi na kwa muda wa majuma matatu akawa anahojiana nao kutoka kwenye Maandiko 3 akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Kristoateswe na afufuke kutoka kwa wafu, akasema, “Huyu Yesu […]

Matendo 18

Paulo Huko Korintho 1 Baada ya haya, Paulo akaondoka Athene akaenda Korintho. 2 Huko akakutana na Myahudi mmoja jina lake Akila, mwenyeji wa Ponto, ambaye alikuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona, 3 naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, […]

Matendo 19

Paulo Huko Efeso 1 Wakati Apolo akiwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, 2 akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” 3 Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.” 4 Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana […]

Matendo 20

Paulo Apita Makedonia Na Uyunani 1 Baada ya kumalizika kwa zile ghasia, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawatia moyo, akawaaga, akaanza safari kwenda Makedonia. 2 Alipopita katika sehemu zile, akinena na watu maneno mengi ya kuwatia moyo, ndipo hatimaye akawasili Uyunani, 3 ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya […]