Zaburi 41

Maombi Ya Mtu Mgonjwa (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) 1 Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwanaatamwokoa wakati wa shida. 2 Bwanaatamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. 3 Bwanaatamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake. 4 Nilisema, “EeBwananihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” 5 Adui zangu […]

Zaburi 42

Maombi Ya Mtu Aliye Uhamishoni (Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora) 1 Kama vile paa aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. 2 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? 3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, huku watu […]

Zaburi 43

Maombi Ya Mtu Aliyeko Uhamishoni Yanaendelea 1 Ee Mungu unihukumu, nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu, niokoe na watu wadanganyifu na waovu. 2 Wewe ni Mungu ngome yangu. Kwa nini umenikataa? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui? 3 Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze; vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka […]

Zaburi 44

Kuomba Ulinzi Wa Mungu (Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora) 1 Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametueleza yale uliyotenda katika siku zao, siku za kale. 2 Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa katika nchi hii na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu. 3 Sio kwa upanga wao waliipata nchi, […]

Zaburi 45

Wimbo Wa Arusi Ya Kifalme (Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora) 1 Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu, ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi. 2 Wewe ni bora kuliko watu wengine wote na midomo yako imepakwa neema, kwa kuwa Mungu amekubariki milele. 3 Jifunge upanga wako pajani mwako, Ee […]

Zaburi 46

Mungu Yuko Pamoja Nasi (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora. Mtindo Wa Alamothi) 1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 2 Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni wa bahari. 3 Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi […]

Zaburi 47

Mtawala Mwenye Enzi Yote (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora) 1 Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe! 2 Jinsi gani alivyo wa kutisha,BwanaAliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote. 3 Ametiisha mataifa chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu. 4 Alituchagulia urithi wetu kwa ajili yetu fahari […]

Zaburi 48

Sayuni, Mji Wa Mungu (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora) 1 Bwanani mkuu na anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu. 2 Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. # Kama vilele vya juu sana vya Safonini Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu. 3 Mungu yuko […]

Zaburi 49

Upumbavu Wa Kutegemea Mali (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora) 1 Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii. 2 Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja: 3 Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu. 4 Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze: 5 […]

Zaburi 50

Ibada Ya Kweli (Zaburi Ya Asafu) 1 Mwenye Nguvu, Mungu,Bwana, asema na kuiita dunia, tangu maawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua. 2 Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza. 3 Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali. 4 Anaziita mbingu zilizo juu na nchi, ili aweze […]