Zaburi 31

Maombi na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui (Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, ninakukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe. 2 Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka, uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa. 3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina […]

Zaburi 32

Furaha Ya Msamaha (Utenzi: Zaburi Ya Daudi. Funzo) 1 Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa. 2 Heri mtu yule ambayeBwana hamhesabii dhambi, na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu. 3 Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa. 4 Usiku na mchana mkono wako ulinilemea, nguvu zangu zilinyonywa […]

Zaburi 33

Ukuu Na Wema Wa Mungu 1 MwimbieniBwanakwa furaha, enyi wenye haki; kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. 2 MsifuniBwanakwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. 3 Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, pigeni kelele za furaha. 4 Maana neno laBwanani haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo. 5 Hupenda uadilifu na haki; dunia […]

Zaburi 34

Sifa Na Wema Wa Mungu (Zaburi Ya Daudi, Alipojifanya Mwendawazimu Mbele Ya Abimeleki, Ambaye Alimfukuza, Naye Akaondoka) 1 NitamtukuzaBwananyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote. 2 Nafsi yangu itajisifu katikaBwana walioonewa wasikie na wafurahi. 3 MtukuzeniBwanapamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. 4 NilimtafutaBwananaye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. 5 Wale […]

Zaburi 35

Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui (Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, pingana na wale wanaopingana nami, upigane na hao wanaopigana nami. 2 Uchukue ngao na kigao, inuka unisaidie. 3 Inua mkuki wako na fumolako dhidi ya hao wanaonifuatia. Uiambie nafsi yangu, “Mimi ni wokovu wako.” 4 Wafedheheshwe na waaibishwe wale wanaotafuta uhai wangu, wanaofanya shauri […]

Zaburi 36

Uovu Wa Mwanadamu (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Mtumishi Wa Mungu) 1 Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. 2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno kiasi kwamba hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. 3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya […]

Zaburi 37

Mwisho Wa Mtu Mwovu (Zaburi Ya Daudi) 1 Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu wala usiwaonee wivu watu watendao maovu, 2 kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara. 3 MtumainiBwanana utende yaliyo mema, ukae katika nchi ukafurahie malisho salama. 4 Jifurahishe katikaBwananaye atakupa haja za moyo wako. 5 MkabidhiBwananjia yako, […]

Zaburi 38

Maombi Ya Mtu Anayeteseka (Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, usinikemee katika hasira yako wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. 2 Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia. 3 Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. 4 Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika. 5 […]

Zaburi 39

Maombi Ya Mtu Anayeteseka (Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yeduthuni. Zaburi Ya Daudi) 1 Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” 2 Lakini niliponyamaza kimya na kutulia, hata pasipo kusema lo lote jema, uchungu wangu uliongezeka. 3 Moyo wangu ulipata moto ndani […]

Zaburi 40

Wimbo Wa Sifa (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) 1 NilimngojaBwanakwa saburi, naye akaniinamia akasikia kilio changu. 2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka katika matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama. 3 Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa […]