1 Mambo ya Nyakati 21

Daudi Ahesabu Wapiganaji 1 Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli. 2 Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.” 3 Yoabu akajibu, “Bwanana aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana […]