Ezekieli 11

Hukumu Juu Ya Viongozi Wa Israeli 1 Ndipo Roho akaniinua na kunileta mpaka kwenye lango la nyumba yaBwanalinalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango kulikuwepo wanaume ishirini na watano, nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu. 2 Bwanaakaniambia, “Mwanadamu, hawa ndio wafanyao hila na […]

Ezekieli 12

Kutekwa Kwa Yuda Kwaelezwa 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Mwanadamu, unaishi miongoni mwa watu waasi. Wana macho ya kuona, lakini hawaoni na masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa kuwa ni watu waasi. 3 “Kwa hiyo, mwanadamu, funga mizigo yako kwa kwenda uhamishoni tena wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toka nje na uende mahali pengine kutoka […]

Ezekieli 13

Manabii Wa Uongo Walaumiwa 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno laBwana! 3 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona cho chote! 4 Manabii wako, Ee Israeli ni kama mbweha […]

Ezekieli 14

Waabudu Sanamu Walaumiwa 1 Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu. 2 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema: 3 “Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lo lote? 4 Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Wakati […]

Ezekieli 15

Yerusalemu Mzabibu Usiofaa 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora zaidi kuliko tawi la mti mwingine wo wote ndani ya msitu? 3 Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza cho chote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuning’inizia vitu kutokana na huo mti wake? 4 Nao […]

Ezekieli 16

Yerusalemu, Mwanamke Asiye Mwaminifu 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Mwanadamu, ijulishe Yerusalemu kuhusu mwenendo wake wa machukizo 3 na useme, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi, analomwambia Yerusalemu: Wewe asili yako na kuzaliwa kwako ni katika nchi ya Kanaani, baba yako alikuwa Mwamori, naye mama yako alikuwa Mhiti. 4 Siku uliyozaliwa kitovu chako hakikukatwa, wala hukuogeshwa kwa maji ili […]

Ezekieli 17

Tai Wawili Na Mizabibu 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo. 3 Waambie hivi, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi, 4 akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika […]

Ezekieli 18

Roho Itendayo Dhambi Itakufa 1 Neno laBwanalikanijia kusema: 2 “Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: “ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu, nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’? 3 “Hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. 4 Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile […]

Ezekieli 19

Maombolezo Kwa Ajili Ya Wakuu Wa Israeli 1 “Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli 2 na useme: “ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike miongoni mwa simba! Alilala katikati ya wana simba na kulisha watoto wake. 3 Alimlea mmoja wa watoto wake, naye akawa simba mwenye nguvu. Akajifunza kurarua mawindo naye akala […]

Ezekieli 20

Israeli Waasi 1 Katika mwaka wa saba, mwezi wa tano siku ya kumi, baadhi ya wazee wa Israeli wakaja ili kutaka ushauri kwaBwana, wakaketi mbele yangu. 2 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema: 3 “Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake […]