Isaya 21

Unabii Dhidi Ya Babeli 1 Neno kuhusu Jangwa kando ya Bahari: Kama upepo wa kisulisuli unaopita katika nchi hadi kusini, mshambuliaji anakuja kutoka jangwani, kutoka katika nchi inayotisha. 2 Nimeonyeshwa maono ya kutisha: Msaliti anasaliti, mteka nyara anateka nyara. Elamu, shambulia Umedi! Izunguke kwa jeshi! Nitakomesha huzuni zote alizosababisha. 3 Katika hili mwili wangu umeteswa […]

Isaya 22

Unabii Kuhusu Yerusalemu 1 Neno kuhusu Bonde la Maono: Nini kinachokutaabisha sasa, kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa? 2 Ewe mji uliojaa ghasia, Ewe mji wa makelele na karamu za sherehe! Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga, wala hawakufa vitani. 3 Viongozi wako wote wamekimbia pamoja, wamekamatwa bila kutumia upinde. Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa […]

Isaya 23

Unabii Kuhusu Tiro 1 Neno kuhusu Tiro: Ombolezeni, Enyi meli za Tarshishi! Kwa kuwa Tiro imeangamizwa, imeachwa bila nyumba wala bandari. # Kuanzia nchi ya Kitimu neno limewajia. 2 Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani, pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao mabaharia wamewatajirisha. 3 Kwenye maji makuu nafaka za Shihori zilikuja; mavuno ya Nile yalikuwa […]

Isaya 24

Dunia Kuharibiwa Upesi 1 Tazama,Bwanaataifanya dunia kuwa ukiwa na kuiharibu, naye atauharibu uso wake na kutawanya wakaao ndani yake: 2 ndivyo itakavyokuwa kwa makuhani na kwa watu, kwa bwana na kwa mtumishi, kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike, kwa muuzaji na kwa mnunuzi, kwa mkopaji na kwa mkopeshaji, kwa mdaiwa na kwa mdai. […]

Isaya 25

Msifuni Bwana 1 EeBwana, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza na kulisifu jina lako, kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu umetenda mambo ya ajabu, mambo yaliyokusudiwa tangu zamani. 2 Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi, mji wenye ngome kuwa magofu, ngome imara ya wageni kuwa si mji tena, wala hautajengwa tena kamwe. 3 Kwa hiyo mataifa […]

Isaya 26

Wimbo Wa Ushindi 1 Katika siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji ulio na nguvu, Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake. 2 Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia, taifa lile lishikalo imani. 3 Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini […]

Isaya 27

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli 1 Katika siku ile, Bwanaataadhibu kwa upanga wake, upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu, # ataadhibu Lewiathaniyule nyoka apitaye mbio kwa mwendo laini, Lewiathani yule nyoka mwenye kupindapinda; atamwua joka huyo mkubwa sana wa baharini. 2 Katika siku ile: “Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa: 3 Mimi,Bwana, ninalitunza, nitalinyweshea […]

Isaya 28

Ole Wa Efraimu 1 Ole wa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu, kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo! 2 Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. Kama dhoruba ya mvua ya mawe na […]

Isaya 29

Ole Wa Mji Wa Daudi 1 Ole wako, wewe Arieli, Arieli, mji alimokaa Daudi! Ongezeni mwaka kwa mwaka na mzunguko wa sikukuu zenu uendelee. 2 Hata hivyo nitauzunguka Arieli kwa jeshi, utalia na kuomboleza, utakuwa kwangu kama mahali pa kuwashia moto madhabahuni. 3 Nitapiga kambi pande zote dhidi yako, nitakuzunguka kwa minara na kupanga mazingiwa […]

Isaya 30

Ole Wa Taifa Kaidi 1 Bwanaasema, “Ole wa watoto wakaidi, kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu, wakifanya umoja, lakini si kwa Roho wangu, wakilundika dhambi juu ya dhambi, 2 wale washukao kwenda Misri bila kutaka shauri langu, wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao, watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio. 3 Lakini ulinzi […]