Kutoka 11

Pigo La Kumi: Kuuawa Wazaliwa Wa Kwanza 1 BasiBwanaalikuwa amemwambia Mose, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa. 2 Waambie watu wote waume kwa wake wawaombe majirani zao vitu vya fedha na vya dhahabu.” 3 (Bwanaakawafanya Wamisri wawe na […]

Kutoka 12

Pasaka 1 Bwanaakamwambia Mose na Aroni katika nchi ya Misri, 2 “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu. 3 Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba. 4 Ikiwa […]

Kutoka 13

Kuwekwa Wakfu Kwa Wazaliwa Wa Kwanza 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua tumbo miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.” 3 Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya […]

Kutoka 14

Kuvuka Bahari Ya Shamu 1 NdipoBwanaakamwambia Mose, 2 “Waambie Waisraeli wageuke nyuma na wapige kambi karibu na Pi-Hahirothi, kati ya Migdoli na bahari. Watapiga kambi kando ya bahari, mkabala na Baal-Sefoni. 3 Farao atafikiri kwamba, ‘Hao Waisraeli wanatangatanga katika nchi kwa kuchanganyikiwa, nalo jangwa limewafungia.’ 4 Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini […]

Kutoka 15

Wimbo Wa Mose Na Miriamu 1 Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbiaBwanawimbo huu: “NitamwimbiaBwana, kwa kuwa ametukuzwa sana. Farasi na mpanda farasi amewatosa baharini. 2 Bwanani nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3 Bwanani shujaa wa vita; Bwanandilo jina lake. 4 Magari […]

Kutoka 16

Mana Na Kware 1 Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka Elimu, wakafika Jangwa la Sini, lililokuwa kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka Misri. 2 Huko jangwani hiyo jumuiya yote ikamnung’unikia Mose na Aroni. 3 Waisraeli wakawaambia, “Laiti tungelikufa kwa mkono waBwanahuko Misri! Huko tuliketi tukizunguka […]

Kutoka 17

Maji Kutoka Kwenye Mwamba 1 Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kamaBwanaalivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. 2 Kwa hiyo wakagombana na Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Mose akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribuBwana?” 3 Lakini watu walikuwa […]

Kutoka 18

Yethro Amtembelea Mose 1 Basi Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wa Mose, akawa amesikia kila kitu Mungu alichomfanyia Mose na watu wake wa Israeli, pia jinsiBwanaalivyowatoa Israeli Misri. 2 Baada ya Mose kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea 3 pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershoni, kwa kuwa Mose alisema, […]

Kutoka 19

Waisraeli Kwenye Mlima Sinai 1 Mnamo mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kuondoka Misri, siku kama iyo hiyo, wakafika katika Jangwa la Sinai. 2 Baada ya kuondoka Refidimu, waliingia katika Jangwa la Sinai na Israeli wakapiga kambi pale jangwani mbele ya mlima. 3 Kisha Mose akakwea kwenda kwa Mungu, nayeBwanaakamwita kutoka kwenye ule mlima akasema, […]

Kutoka 20

Amri Kumi 1 Ndipo Mungu akasema maneno haya yote: 2 “Mimi ndimiBwanaMungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 5 Usivisujudie au kuviabudu; kwa kuwa Mimi,BwanaMungu wako, […]