Kutoka 31

Bezaleli Na Oholiabu 1 NdipoBwanaakamwambia Mose, 2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na maarifa katika aina zote za ufundi, 4 ili kubuni kazi za ustadi katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 5 kuchonga vito vya kutia […]

Kutoka 32

Ndama Ya Dhahabu 1 Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.” 2 Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” 3 Kwa hiyo watu wote […]

Kutoka 33

Amri Ya Kuondoka Sinai 1 KishaBwanaakamwambia Mose, “Ondoka mahali hapa, wewe pamoja na hao watu uliowapandisha kutoka Misri, mpande mpaka nchi niliyomwahidi Abrahamu, Isaki na Yakobo kwa kiapo, nikisema, ‘Nitawapa wazao wenu nchi hii.’ 2 Nitamtuma malaika mbele yenu, naye atawafukuza Wakanaani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 3 Pandeni mwende katika nchi itiririkayo maziwa […]

Kutoka 34

Vibao Vipya Vya Mawe 1 Bwanaakamwambia Mose, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. 2 Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. 3 Mtu ye yote asije pamoja nawe, […]

Kutoka 35

Masharti Ya Sabato 1 Mose akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndiyo mambo ambayoBwanaamewaamuru ninyi mfanye: 2 Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya kupumzika kwaBwana. Ye yote atakayefanya kazi yo yote siku hiyo ni lazima auawe. 3 Msiwashe moto mahali po pote katika makazi yenu […]

Kutoka 36

1 Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtuBwanaaliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vileBwanaalivyoagiza.” 2 Ndipo Mose akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambayeBwanaalikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi. 3 Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka […]

Kutoka 37

Sanduku La Agano 1 Bezaleli akatengeneza Sanduku kwa mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. 2 Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. 3 Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake […]

Kutoka 38

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa 1 Akatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu;nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano na upana wa dhiraa tano. 2 Akatengeneza upembe kwenye kila pembe katika hizo pembe nne, ili kwamba zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. […]

Kutoka 39

Mavazi Ya Kikuhani 1 Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Aroni mavazi matakatifu, kamaBwanaalivyomwagiza Mose. Kisibau 2 Akatengeneza kisibau kwa nyuzi za rangi ya dhahabu, ya buluu, ya zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri. 3 Akafua […]

Kutoka 40

Kusimika Maskani Ya Mungu 1 KishaBwanaakamwambia Mose: 2 “Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. 3 Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake. 4 Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake. […]