Luka 11

Yesu Afundisha Wanafunzi Wake Kuomba 1 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tufundishe kuomba, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.” 2 Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje. 3 Utupatie kila siku riziki zetu. 4 Utusamehe dhambi zetu, […]

Luka 12

Maonyo Dhidi Ya Unafiki 1 Wakati huo, umati mkubwa wa watu kwa maelfu, walipokuwa wamekusanyika, hata wakawa wanakanyagana, Yesu akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao. 2 Hakuna jambo lo lote lililositirika ambalo halitafunuliwa au lililofichwa ambalo halitajulikana. 3 Kwa hiyo, lo lote mlilosema gizani litasikiwa nuruni […]

Luka 13

Tubu, La Sivyo Utaangamia 1 Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Yesu habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa. 2 Yesu akawauliza, “Mnadhani kwamba hawa Wagalilaya ambao walikufa kifo cha namna hiyo wao walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 3 La hasha! Ninyi […]

Luka 14

Yesu Nyumbani Mwa Farisayo 1 Ikawa siku moja Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo siku ya Sabato, watu walikuwa wakimchunguza kwa bidii. 2 Papo hapo mbele yake palikuwa na mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba mwili. 3 Yesu akawauliza wale Mafarisayo na walimu wa sheria, “Je, ni halali kuponya watu […]

Luka 15

Mfano Wa Kondoo Aliyepotea 1 Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Yesu. 2 Lakini Mafarisayo na walimu wa sheria wakanung’unika wakisema, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao.” 3 Ndipo Yesu akawaambia mfano huu: 4 “Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi […]

Luka 16

Mfano Wa Msimamizi Mjanja 1 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na msimamizi wake. Ilisemekana kwamba huyo msimamizi alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. 2 Hivyo huyo tajiri akamwita na kumwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’ 3 “Yule msimamizi akawaza […]

Luka 17

Yesu Afundisha Kuhusu Majaribu, Dhambi Na Imani 1 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. 2 Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutoswa baharini kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi. 3 Kwa hiyo, jilindeni. “Kama ndugu […]

Luka 18

Mfano Wa Mjane Asiyekata Tamaa 1 Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa. 2 Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3 Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui […]

Luka 19

Zakayo Mtoza Ushuru 1 Yesu akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. 2 Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. 3 Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Yesu ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. […]

Luka 20

Wahoji Kuhusu Mamlaka Ya Yesu 1 Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wakamjia. 2 Wakamwuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?” 3 Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. 4 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa […]