Mithali 11

1 Bwanahuchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake. 2 Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. 3 Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao. 4 Utajiri haufaidii kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. 5 Haki ya wasio na lawama, […]

Mithali 12

Mafundisho Ya Kifamilia Na Ya Kijamii 1 Ye yote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa, bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu. 2 Mtu mwema hupata kibali kutoka kwaBwana, baliBwanahumhukumu mwenye hila. 3 Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa. 4 Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa […]

Mithali 13

Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu 1 Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye, bali mwenye dharau hasikilizi maonyo. 2 Kutoka katika tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema, bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri. 3 Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake, bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia. 4 Mvivu hutamani […]

Mithali 14

1 Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. 2 Yeye ambaye njia zake ni nyofu humchaBwana, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. 3 Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake, bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. 4 Pale ambapo hakuna mafahali, hori […]

Mithali 15

1 Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. 2 Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. 3 Macho yaBwanayako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. 4 Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho. 5 Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali ye […]

Mithali 16

1 Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwaBwana. 2 Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa naBwana. 3 MkabidhiBwanalo lote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. 4 Bwanahufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe, hata waovu kwa siku ya maangamizi. 5 Bwanahuwachukia sana wote wenye kiburi […]

Mithali 17

1 Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi. 2 Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. 3 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, baliBwanahuujaribu moyo. 4 Mtu […]

Mithali 18

1 Mtu ajitengaye na wengine hufuata matakwa yake mwenyewe; hupiga vita kila shauri jema. 2 Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe. 3 Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia, pamoja na aibu huja lawama. 4 Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika. 5 Sio […]

Mithali 19

1 Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. 2 Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. 3 Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake pamoja na hivyo moyo wake humkasirikiaBwana. 4 Mali huleta marafiki wengi, bali rafiki wa mtu maskini humwacha. 5 […]

Mithali 20

1 Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; ye yote apotoshwaye navyo hana hekima. 2 Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. 3 Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. 4 Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati […]