Mithali 21

1 Moyo wa mfalme uko katika mkono waBwana; huuongoza kama mkondo wa maji, po pote apendapo. 2 Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, baliBwanahuupima moyo. 3 Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwaBwanakuliko dhabihu. 4 Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi! 5 Mipango ya […]

Mithali 22

1 Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi, kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu. 2 Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: Bwanani Muumba wao wote. 3 Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa. 4 Unyenyekevu na kumchaBwana huleta utajiri, heshima na uzima. 5 Katika mapito ya […]

Mithali 23

1 Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako, 2 na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi. 3 Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. 4 Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonyesha kujizuia. 5 Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka […]

Mithali 24

1 Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; 2 kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta taabu. 3 Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa, 4 kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. 5 Mtu mwenye hekima ana […]

Mithali 25

Mithali Zaidi Za Solomoni 1 Hizi ni mithali zaidi za Solomoni, zilizonakiliwa na watu wa Hezekia mfalme wa Yuda: 2 Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. 3 Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. 4 Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, […]

Mithali 26

1 Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu. 2 Kama shomoro apigapigavyo mbawa zake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu. 3 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu! 4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, […]

Mithali 27

1 Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. 2 Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe. 3 Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito zaidi kuliko hivyo vyote viwili. 4 Hasira ni […]

Mithali 28

1 Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna ye yote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba. 2 Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. 3 Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao. 4 Wale waiachao sheria huwasifu waovu, bali […]

Mithali 29

1 Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, wala hapati dawa. 2 Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. 3 Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na kahaba hutapanya mali yake. 4 Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na […]

Mithali 30

Mithali Za Aguri 1 Mithali za Aguri mwana wa Yake, mausia: Huyu mtu alimwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali: 2 “Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu. 3 Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu. 4 Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya […]